Posts

Showing posts from June 19, 2022

MAOMBI USHTUKAPO NDOTONI

 MAOMBI USHTUKAPO NDOTONI (NDOTO MAJIBU) Unapo-amka usingizini sikuzako zote, usingizi wa ndoto yaani mfurulizo wa matukio wakati umelala kitandani/popote ulipo sinzia, kwanza usinung'unike mbele za Mungu kana kwamba Mungu hakupendi wewe, au ameruhusu ndoto ya namna hiyo ikupate kwanini hilo litokee kwako. Maandiko husema, Ayubu 33 (Biblia Takatifu) ¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯ ¹⁴ Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. ¹⁵ Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; ¹⁶ Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Pia neno linazidi kueleza Ninini kusudi la ndoto husika, Ayubu 36 (Biblia Takatifu) ¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯ ⁹ Ndipo huwaonyesha matendo yao, Na makosa yao, ya kuwa wametenda kwa kujivuna. ¹⁰ Yeye huyafunua masikio yao, wasikie maonyo, Na kuwaagiza warudi kuuacha uovu. ¹¹ Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha. ¹² Lakini wasiposikia, wat