MAOMBI USHTUKAPO NDOTONI

 MAOMBI USHTUKAPO NDOTONI

(NDOTO MAJIBU)


Unapo-amka usingizini sikuzako zote, usingizi wa ndoto yaani mfurulizo wa matukio wakati umelala kitandani/popote ulipo sinzia, kwanza usinung'unike mbele za Mungu kana kwamba Mungu hakupendi wewe, au ameruhusu ndoto ya namna hiyo ikupate kwanini hilo litokee kwako.

Maandiko husema, Ayubu 33 (Biblia Takatifu)

¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯

¹⁴ Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.

¹⁵ Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;

¹⁶ Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,


Pia neno linazidi kueleza Ninini kusudi la ndoto husika, Ayubu 36 (Biblia Takatifu)

¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯

⁹ Ndipo huwaonyesha matendo yao, Na makosa yao, ya kuwa wametenda kwa kujivuna.

¹⁰ Yeye huyafunua masikio yao, wasikie maonyo, Na kuwaagiza warudi kuuacha uovu.

¹¹ Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha.

¹² Lakini wasiposikia, wataangamia kwa upanga, Nao watakufa pasipo maarifa.


Hivyo Muota ndoto husika anapaswa kuingia/KUANZA maombi haraka anaposhtuka katika ndoto yake, na anapaswa kuomba kulingana na Maandiko/Neno la Mungu, Ili kudhihirisha ni kweli umekusudia kuukabidhi moyo/maisha yako Kwa kristo naye akusaidie kuondoka uangamivu ambao Mungu mwenyewe amekuonyesha Ili akuondoe katika huo.

KUMBUKA HILI SANA.....sio kwamba MUNGU anashindwa kukutoa/kukuepusha bila wewe binafsi kujua HAPANA ila anacho hitaji Mungu kwako ni PATANO KATI YAKO NA MUNGU Ili usitende dhambi ukarudia hali ngumu Tena.


MUOMBE MUNGU MAMBO HAYA....

1.Utakaso

    Yaani Mungu akuondolee makosa yako akusafishe dhambi zako, omba Kwa jina la Bwana Yesu Kristo, maana Mungu husikia wamwombao hasa kwaimani juu ya Mwana,Baba(Mungu) na Roho Mtakatifu. 

HAKIKISHA UNAOMBA MPAKA UNASIKA AMANI NDANI YA MOYO WAKO.


2.Omba kuelewa ujumbe wa Mungu uliomo ndani ya ndoto yako. (Uliona vyema shirikisha watumishi wa Mungu {PastorChrismyeya±255786620305 whatsapp elezea ndoto yako} mweleze Mungu amjuze mtumishi wake kuhusu ndoto yako katika kuomba kwako) Hakikisha ukiweza kuingia maombi kutilia mkazo na kumpa thamani/nafasi ya kwanza Mungu wetu.


3.Omba REHEMA na KIBALI KWA MUNGU.

Uhakikishe unamwambia Mungu akurehemu, maana bila rehema ya Mungu huwezi sogea popote, KUMBUKA, asilimia kubwa Mungu huzungumza na wanadamu katika ndoto Ili kuwaokoa na kuzimu/mauti/shida,mateso,taabu/usienda shimoni,upotevuni. Hivyo rehema inakupa kukaribiana Tena na Mungu kama ulijitenga pamoja na pendo lake.


4.Shukrani Kwa Mungu.

Mshukuru Mungu Kwa kukuonyesha hilo na kusema nawe (KUMBUKA;-Shukuru Mungu hata kama bado hujapokea majibu) UKIWEZA AMBATANISHA SHUKRANI YAKO NA SADAKA YAKO YA SHUKRANI, Kwa mtumishi aliyekua pamoja nawe katika suala hilo, Ili MUNGU aendelee kuhusika sadaka Huwa ni muhuri wa pekee.


5.Hakikisha unamkabidhi Bwana Yesu maisha yako, Mungu yeye husema zaidi na wanawe walio mpokea, endapo hukuokika, Huwa Mungu anataka akuokoe, hivyo hakikisha Kwa usalama wa maisha yako zaidi kumpokea Bwana Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha yako na usimuache kabisa Yesu. AMINA.


BWANA YESU NI MUWEZA ATAKUPA TAFSIRI KAMILI YA NDOTO YAKO.

PastorChrismyeya.+255786620305

UBARIKIWE.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAWI KIUHALISIA

NDOTO NA MAANA ZAKE

UHALISIA ROHONI