Posts

Showing posts from February 25, 2024

AINA TATU ZA MAUTI

AINA TATU ZA MAUTI NA NGUVU ILIYOMO NDANI YA HIYO AINA YA MAUTI. Mauti hasa ni Nini? U-Mauti ni Kifo. MAUTI ni hali au kitendo cha mtu kutoka katika uhai kuingia KIFO/KUFA (Mfano wa msemo; Umauti ulimkuta akiwa safarini kuja hapa! (ni kitendo). U-mauti unapo mjia mtu huwa anashindana nao pasipo kujua ki-mwili, wengine huaga wapendwa wao Kwa hali kanakwamba ni fumbo asilolijua hata muagaji anaye aga. KIFO/KUFA ni kutokua na mawasiliano kabisa kati ya mwili na roho, yaani ni hali ya milango ya fahamu kutofanya kazi tena kabisa na kuanza kuharibika, moyo kushindwa kuendelea na kazi yake ya kusukuma damu hivyo mwilini damu huganda na hapo ndipo ulipo mwisho wa uzima wa mwili huu. ( wakati huo roho ya mwanadamu huendelea kuishi ) AINA ZA MAUTI 1.MAUTI YA KWANZA. >Huua mwili (Mwili kuachana na Roho) 2.MAUTI YA PILI. > Roho kuhukumiwa adhabu ya moto. 3.MAUTI YA TATU. >Mtu anaishi/anapumua, ila hampendezi Mungu. somo Lina endeleaaa.........

AINA TATU ZA MAUTI

AINA TATU ZA MAUTI NA NGUVU ILIYOMO NDANI YA HIYO AINA YA MAUTI. Mauti hasa ni Nini? Mauti ni mwili ulio KUFA. MAUTI ni hali au kitendo cha mtu kutoka katika uhai kuingia KIFO/KUFA (Mfano wa msemo; Umauti ulimkuta akiwa safarini kuja hapa! (ni kitendo). U-mauti unapo mjia mtu huwa anashindana nao pasipo kujua ki-mwili, wengine huaga wapendwa wao Kwa hali kanakwamba ni fumbo asilolijua hata muagaji anaye aga. KIFO/KUFA ni kutokua na mawasiliano kabisa kati ya mwili na roho, yaani ni hali ya milango ya fahamu kutofanya kazi tena kabisa na kuanza kuharibika. AINA TATU ZA MAUTI

NABII NI NANI KI-BIBLIA?

 JINSI YA KUWATAMBUA MANABII WA KWELI. Katika somo hili nitaelezea jinsi ya kuwatambua manabii wa kweli wa Mungu kutokana na sifa walizokuwa nazo wakati wa Agano la Kale na Agano Jipya. Ni muhimu kila mkristo aliyeokoka aweze kupambanua (kutofautisha) na kutambua manabii wa kweli na manabii wa uongo. Manabii wa kweli walikuwa na sifa zifuatazo; 1.Walikuwa waaminifu. Hapa tutaangalia manabii watatu ambao ni Yesu, Musa na Samweli ambao walikuwa waaminifu katika mambo yote ya Mungu. Waebrania 3:1-2 “...Yesu aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama naye Musa alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.” Katika andiko hili, Yesu amefananishwa na nabii Musa alivyokuwa mwaminifu. Mwingine ni Samweli, alipokuwa mzee aliwashuhudia wana wa Israel jinsi alivyokuwa mwaminifu tangu akiwa kijana. 1Samweli 12:2-4 “Basi sasa, angalieni, mfalme anakwenda mbele yenu; na mimi ni mzee, mwenye mvi; tena, tazameni, wana wangu wapo pamoja nanyi; nami nimekwenda mbele yenu toka ujana wangu hata leo.