MKONO IMARA WA KUUAMINI

  https://www.googletagmanager.com/gtm.js?id='+i+dl;f.parentNode.insertBefore(j,f);
})(window,document,'script','dataLayer','GTM-T7RRGW4F');</script>
<!-- End Google Tag Manager -->   Nnamshukuru sana MUNGU katika KRISTO YESU alienipa mamlaka na uwezo wa kuandika makala hii, nnasema JINA LA BWANA WANGU, YESU KRISTO NA LIHIMIDIWE DAIMA.
   KRISTO YESU na ushukuriwe kwakunipa kibali hiki cha makala hii ambayo inalenga kuyarudisha ya mkristo katika mstari mnyoofu wa maisha yako uliotuasa kuyaishi katika ulimwengu huu tuliopo. Nikweli ulimwengu uko vilevile ispokua waishio ulimwenguni (wanadamu) baadhi yao wanakwenda kinyume na kufuata taratibu za ibilisi shetani kwaajili ya kulitukana jina lako Jehovah, (tuhurumie maana shetani amejivika mbinu zakutosha TUSAIDIE EEE YESU KRISTO WA NAZARETI)
   Basi fuatilia makala hii na miendelezo take ili kwanba wewe ndugu katika KRISTO YESU na ambae bado hujampokea kristo YESU akusaidie sikumoja uione mbingu, watakatifu na zaidi kwenda kumuona mwanakondoo aliekufa kwaajili ya dhambi za wanadamu wote.
                     AMEN
   Tena mojakwamoja nikushirikishe kuhusu MKONO IMARA WA KUUAMINI; huu  ni mkono ambao unanguvu za kutosha kushinda Jambo/mambo magumu/mazito ambayo kwa kawaida pekeyako huwezi kuyashinda, maanayake unahitaji MSAADA kutoka sehemu nyingine yakuweza kukusaidia ili kusimama tena/kua na tumaini jipya la uhakika.
   Kwa haraka tu! Nnataka kukuhakikishia, hakuna MKONO IMARA WAKUUAMINI popote ISPOKUA  mkono wa MUNGU BABA na "YESU MWANAE" hivyo mkono huu wa MUNGU ndio pekee wakuaminiwa na wanadamu wote ulimwenguni:
      Hivyo basi nimekuandikia wewe kijana/binti/mama/baba. Pia, yatima/mjane/mgane na nk.... Kwamba hupaswi kuona  hapo ulipo huwezi tena kuendelea, nnakufungua tu kimawazo kwamba hapo ulipo sasa ni sehemu nzuri ya kumtaka MUNGU ajidhihirishe kwako kwa viwango vikubwa na vyakushangaa matendo aliokuandalia kuyaona kwa machoyako mwenyewe (binafsi) ili usimulie habari za ukuu wake "MUNGU" endapo tu utachukua hatua; kamwe usivunjike moyo...
Hatakama kunawakati unafika pekeyako huwezi kwenda au kufanya lolote na unahitaji msaada katika kushinda hilo ambalo umeshindwa kulifanya pekeyako, nduguyangu mikononi mwa MUNGU ndiko pekee patakufanya uwe salama na kukupandisha viwango vikubwa mnoooo... HEBU KUMBUKA wakati yesu alipokua akisali katika,   Luka : 23
46 Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu. (Ni nguvu gani iliopo mikononi mwa MUNGU? jiulize, JE! wakati YESU alipokua akisema maneno hayo mbele za MUNGU alikua katika wakati wa raha na kustarehe? Kwanini wewe usahau kujiweka mikononi mwa mungu kwa uhakika kwamba anaweza?)
Na utaona tena wakati huo unakua wakati mbaya/mgumu wakimawazo na hasa katika kuamua mambo ya msingi yenye hatima ya kimaisha, maana unakua katika hali yakuto weza lolote pasipo msaada, tena msaada wenye kusaidia yaani MSAADA IMARA. Kwa wakati huo. (kumbuka msaada imara u katika MUNGU pekee mwanadamu hawezi wala mizimu/mashetani hayawezi) lakini Mtunga zaburi anasema....Zaburi :  31
5 Mikononi mwako naiweka roho yangu;Umenikomboa, Ee BWANA, Mungu wa kweli. Ooooh, ni nguvu gani hii ilioko mikononi mwako MUNGU wangu wa Israeli.
Pia katika wakati huo Ipo mikono itanyooshwa kwako ya kukusaidia ili kutaka kukutoa ulipo, Mfano; nipale ambapo shetani alipokuwa akimjaribu Yesu kristo mwenyewe ( Imeandikwa katika;Mathayo :  4. 6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa,Atakuagizia malaika zake;Na mikononi mwao watakuchukua;Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. (Hivyo shetani anajua fika/kabisa kwamba MUNGU anayo mikono imara yakuweza kumkinga yesu na asianguke/kudondoka {lakini yesu hakufanya hivyo maana alitambua kua ni jaribu mbeleyake na} pia ukumbuke shetani pia hapo alisha mdanganya YESU pia akamwambia malaika ndio watakaomdaka kwa mikono yao NO shetani anasimamia neno kukupata "kuamakini analikwepesha neno")
Sasa basi, chamsingi unachotakiwa kukitambua haraka sana;
SI KILA MKONO UNAWEZA KUKUSAIDIA, MIKONO MINGI INAUA KABISA, hapo ndipo pakua makini sana! tena sana
KWANINI INAINUKA MIKONO MINGINE KUTAKA KUNISAIDIA?
MATHAYO, 4
1 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.
Kwa mantiki hiyo MUNGU anairuhusu mikono kadha wa kadha kupitia shetani(mjaribu) ili akujaribu na mikono hiyo si salama ni kwasababu tu! Roho wa MUNGU (MUNGU MWENYEWE) ambaye mwenye mkono uliosalama aweze kuipima imani uliokuanayo; (Mithali :  16
2 Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;Bali BWANA huzipima roho za watu.) {ukumbuke roho ndio itendayo dhambi na ndio inayoshawishiwa kufanya lolote lile ili kutenda yalio mabaya yamchukizayo MUNGU (Ezekieli : 18
20 Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa;)
   KWANINI MUNGU ANARUHUSU UJARIBIWE?
MUNGU anamruhusu shetani (mjaribu) kukujaribu ili aone na kujihakikishia/kujiridhisha kwamba, upendo ulionao umezama zaidi wapi? Kwa shetani (mjaribu) au kwake yeye MUNGU MWENYE NGUVU. Ijapokua utajiuliza MUNGU hutambua nia ya kila mmoja wetu kwann anijaribu? Ni kweli MUNGU hutambua nia lakini anaruhusu ujaribiwe ili kuiweka imani yako sawa na kujihakikishia kwamba yeye MUNGU ndiye mwenye thamani kwenye maishayako.
Na ndiomaana basi, mkono wa Bwana MUNGU  wenye nguvu, ili kuipima imani uliokuanayo, unaweza kukutoa hapo ulipo na kukupeleka mahali ili kuipima imani uliokuanayo na kuikuza.
   Imeandikwa;
EZEKIL, 37
1 Mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya BWANA, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa; (Yote hii ni ili tu SIFA na UTUKUFU vivume kwaajili yake MUNGU MWENYE NGUVU)
Hebu fikiria kidogo "endapo kama Ibahimu asinge jaribiwa Leo hii angekua babayetu? Na ni nani alimjaribu? 'SASA KWANINI UNALALAMIKA MACHONI PA MUNGU KILA WAKATI KWA HAPO UNAPOPITIA?, Kwanini usiuhitaji mkono wa MUNGU kukuvusha hapo na sio huko KULALAMIKA?'
Tena zipo faida nyingi mnooo ukiutafuta na kuutaka MKONO IMARA WA MUNGU kwenye maisha yako.
FAIDA ZILIZOPO KWENYE MKONO IMARA WA MUNGU
@UTAKWEZWA utawekwa juu yaani kama kinara kimulikacho/kioo, yaani mfano wakuigwa na watu wengi katika nyanja za namna tofauti kadri MUNGU atakavyokupa kibali.
   Imeandikwa;
1 petro : Mlango 5
6 Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;
  @ Kuwaweka adui zako kimya na kuwatuliza wakamshangaa MUNGU kwa matendo makuu na wewe ukiwa kinara kwao.
     Imeandikwa;
      Mathayo  22:44
"Bwana alimwambia Bwana wangu,Uketi mkono wangu wa kuume,Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?"
@Mkono wa MUNGU wenye nguvu ya ajabu unao uwezo wa kukutoa katika vifungo ulivyonavyo na kukuweka huru kabisa.
      Imeandikwa;
     KUMBUKUMBU LA TORATI 7
8 bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.
@Ukiwa chini ya mkono imara wa bwana MUNGU unakua na mamlaka ulimwenguni popote wa kufanya kila jambo na unakua na nguvu ja ajabu kama mkonowake ulivyo hodari kwa nguvu hizo.
     Imeandikwa;
Luka : Mlango 4
18 Roho wa Bwana yu juu yangu,Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema.Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao,Na vipofu kupata kuona tena,Kuwaacha huru waliosetwa, (kumbuka kwamba palipo roho wa bwana ndipo hapo penye mkono imara wa MUNGU mwenyewe)
YOTE kwa YOTE niseme kwamba unahitaji kivuri cha mkono wa MUNGU kwa viwango vikubwa mnooo
     (heavenlysonofchrist01@gmail.com)https://www.googletagmanager.com/gtm.js?id='+i+dl;f.parentNode.insertBefore(j,f);
})(window,document,'script','dataLayer','GTM-T7RRGW4F');</script>
<!-- End Google Tag Manager -->

Comments

Popular posts from this blog

UCHAWI KIUHALISIA

NDOTO NA MAANA ZAKE

UHALISIA ROHONI