KURUDI KWA YESU MARA YA PILI SEHEMU YA KWANZA
KURUDI KWA YESU MARA YA PILI SEHEMU YA KWANZA
Ujio wa Yesu kwa mara ya kwanza kama kulivyotabiriwa kulikamilika kwa kupitia kuzaliwa na bikira Mariamu. Aliishi kwa makusudi maalumu ya kuleta ukombozi kwa njia ya kifo pale msalabani (Marko 10:45). Wakati maisha na huduma yake hasa wiki ya mwisho aliongea habari za kuondoka lakini kwamba angerudi tena (Yohana 14:1-4; Mathayo 24:4-31). Baada ya kumaliza kazi hiyo msalabani alipaa na kwenda kwa Mungu Baba na malaika waliwakumbusha wanafunzi wake kwamba huyo Yesu waliyemwona anapaa atarudi tena (Matendo 1:11).
Kurudi kwa Yesu ni fundisho la msingi la imani ya kikristo ambalo ni tumaini lenye baraka. Fundisho hili huleta hamasa na shauku ya kumngoja Yesu kwa hofu na utakatifu hali tukimtumikia Mungu kwa juhudi kwa sababu ushirika wa sasa na Kristo una uhusiano na matokeo makubwa sana katika maisha yajayo ya milele. Kuja kwa Yesu mara ya pili
vi | F a h a m u K u h u s u K U R U D I K W A Y E S U
na kuanzisha ufalme wa miaka 1000 ni mwanzo wa Mungu kutekeleza mpango wake wa kuishi na mwanadamu aliyemuumba. Unaposoma kitabu hiki Roho Mtakatifu akusaidie kutafakari juu ya ufupi wa maisha hapa duniani, umuhimu wa kuwekeza katika ufalme wa Mungu na uwe na utayari kwa ajili ya unyakuo wa pamoja au unyakuo binafsi kwa njia ya kifo.
1 | F a h a m u K u h u s u K U R U D I K W A Y E S U
SURA YA KWANZA
MPANGO WA MUNGU WA KUISHI NA MWANADAMU
Hapo Mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi kama Neno lina vyotuelezea katika Mwanzo 1:1. Baada ya kukamilisha uumbaji Mungu ameendeleza kuitunza (Nehemia 9:6) au kuiendesha dunia. Kama kuna mwanzo wa dunia ni lazima kuna mwisho pia. Biblia inatuthibitishia kuwepo kwa mwisho wa dunia na juu ya siku za mwisho. Ni vyema kuamini juu ya mtazamo na fundisho hilo kwa sababu mambo mengi ambayo neno limeyaeleza yalitimia kama neno lilivyosema.
Baadhi ya ushahidi wa kuwepo kwa siku za mwisho tunaupata kupitia maandiko yafuatayo:
i. Yesu, “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja” (Mathayo 24:14).
2 | F a h a m u K u h u s u K U R U D I K W A Y E S U
ii. Mtume Paulo, “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; (1 Timotheo 4:1).
iii. Mtume Paulo, “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari” (2 Timotheo 3:1).
iv. Mtume Yohana, “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho” (1 Yohana 2:18).
v. Yuda, “Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo, ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu” (Yuda 1:17-18).
Ushahidi huu wa maandiko unaonesha kuwa mwisho upo. Sifa au tabia moja kubwa ya msingi kuhusu neno la Mungu ni kuhusu utimilifu wa jambo ambalo neno linasema.
Mifano ni mingi sana juu ya yale ambayo Neno la Mungu lilinena na yakatimia. Mfano mmoja kati ya mingi tunaupata katika kitabu cha Obadia 1:17 “Wala hata salia mtu awayeyote katika nyumba ya Esau kwa kuwa Bwana amesema hayo”.
Utimilifu wa maneno haya tunauona katika ukweli kwamba leo hii hakuna kabisa uzao wa Esau duniani, lakini uzao wa
3 | F a h a m u K u h u s u K U R U D I K W A Y E S U
Yakobo upo ambao ni Taifa la Israeli, kama Neno lilivyosema “Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa Bwana amesema haya”
Tunaposoma kitabu cha Ufunuo 21:1-4 baada ya hukumu zote na Mungu kumalizana na uovu na waovu, sasa atafanya makazi yake na mwanadamu kwa kuwa na ushirika naye kama ilivyokuwa kabla ya anguko.
Kabla ya kufikia hali hiyo ya Mungu kufanya makao na mwanadamu, mambo yafuatayo huwa yanatokea au yatatokea;
MWISHO WA MTU BINAFSI KUPITIA KIFO
Tunapoongea juu ya siku za mwisho tunalazimika kutambua kuwa kuna miisho ya aina mbili.
Mwisho wa kwanza wa maisha ni pale mwanadamu anapokufa. Hapa mwanadamu huwa amefikia mwisho wa maisha yake (personal end). Pia upo mwisho wa jumla kwa dunia nzima (cosmic end) kama maandiko yanavyo thibitisha, “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja (Mathayo 24:14)”.
Mwisho huu wa ujumla ndio utaleta mwisho wa maisha haya ya kawaida yenye masumbuko mengi kuhusu kula, kunywa
4 | F a h a m u K u h u s u K U R U D I K W A Y E S U
na kuvaa, maisha ya kuugua na kufa, maisha ya uchungu na huzuni, maisha ya mapambano kwa ajili kujenga, kusomesha watoto, kuweka akiba kwa ajili ya baadae nk.
WAFU HUENDA WAPI?
Kifo ni hali ya roho na nafsi ya mwanadamu kutengana na mwili. Kibiblia hii huitwa mauti ya kwanza. Kifo ni matokeo ya uasi wa Adamu. Kabla ya mwanadamu hajaanguka katika dhambi, Mungu alimuonya Adamu kuwa siku akila tunda atakufa hakika, “Mwanzo 2:7-3:19”.
Kifo cha kimwili hutokea pale roho ya mwanadamu inapotengana na mwili. Kifo cha mwili kilianza baada ya mwanadamu kumuasi Mungu. Baada ya roho kutengana na mwili roho hiyo huenda kuwa na Mungu kama mtu huyo alipatanishwa na Mungu kwa njia ya wokovu katika Yesu Kristo. Endapo roho hiyo haikupatanishwa na Mungu basi roho hiyo hutengana na Mungu milele.
Mwandishi Herman Hoyt1 ametoa ufafanuzi wa kutosha kuhusu sehemu ambayo wafu huenda wakati wakisubiri kufufuliwa.
Watu waliokufa kuanzia wakati wa Adamu hadi kabla ya kifo cha Yesu walienda kuzimu. Maandiko kadhaa katika Agano la kale yanathibitisha juu ya kuzimu kuwa ni eneo walikokwenda wafu (Mwanzo 25:8-9; Mwanzo 37:35;
1 Herman Hoyt: Endtimes, uk. 34-48
5 | F a h a m u K u h u s u K U R U D I K W A Y E S U
Ayubu 14:13, Zaburi 16:10, Zaburi 86:13, Isaya 38:10; Matendo 2:27,31).
Kwa mujibu wa Andrew McDearmid2, kuzimu ilikuwa imegawanyika katika maeneo mawili; Kuzimu ya juu (upper Sheol) na kuzimu ya chini (lower sheol).
Kuzimu ya chini (lower Sheol) ni sehemu ya mateso, na waovu na wasio mcha Mungu wa nyakati zote huenda kuzimu ya chini (Kumbukumbu 32:22; 2 Petro 2:9; Luka 16:22-24).
Wacha Mungu wa Agano la kale walipokufa walienda kuzimu ya juu ambako palikuwa mahali pa raha na utulivu (1 Samweli 28:15, Danieli 12:13,).
Kuzimu ya juu pia paliitwa kifuani pa baba Ibrahimu (Luka 16:22).
Ni kuzimu ya juu ndiko Yesu alikoshuka alipokufa msalabani (Luka 23:43).
Sehemu hizi mbili zilitenganishwa na shimo kubwa ambalo haiwezekani kuvuka kwa yeyote kutoka upande wowote (Luka 16:23-27).
2 Andrew McDearmid: Eschatology-Independent Study Guide, uk. 5470.
MPANGILIO WA KUZIMU BAADA YA YESU KUFUFUKA
Wanazuoni Herman Hoyt na Andrew McDeamid3 wanaandika kwamba, Yesu alipokufa alienda kuzimu kuwathibitishia wafu wa nyakati zote kwamba yeye ndiye aliyetabiriwa na manabii kuwa angekuja (1 Petro 3:18-20).
Kwa wafu waliokuwa wacha Mungu kushuka kwa Yesu kuzimu ilikuwa ni habari njema kwani alienda kuwafungua kutoka kuzimu (Luka 4:18; 1 Petro 4:8) na kuwahamisha kwenda paradiso ya mbinguni kama ilivyokuwa imetazamiwa tangu Agano la kale (Hosea 13:14, Mithali 15:24). Kwa waovu tangazo la Yesu kule kuzimu lilikuwa ni
k u z i m u
Kuzimu ya chini walikoenda wasiomcha Mungu, wasio haki. Luka 16:23-24
Kuzimu ya juu walikoenda wacha Mungu wenye haki. Luka 16:22; 1 Samweli 28:15
7 | F a h a m u K u h u s u K U R U D I K W A Y E S U
uthibitisho wa hukumu yao na kwamba hakuna wokovu tena kwao.
Baada ya Yesu kufufuka alileta mabadiliko kwa kuwahamisha wacha Mungu waliokuwa kuzimu ya juu (upper Sheol) na kuwahamishia mbinguni au paradiso ya juu (Waefeso 4:8-10).
Wakati Yesu alipofufuka, watakatifu wa Agano la kale walifufuka na kuonekanaYerusalemu. Inaaminika kwamba huu ulikuwa ni mchakato wa kuwahamisha watakatifu toka kuzimu na kuwapeleka mbinguni au paradiso ya juu (Mathayo 27:50-53).
Mtume Paulo anashuhudia kuhusu paradiso iliyopo mbinguni kupitia 2 Wakorintho 12:1-4, ambako kwa neema ya Mungu alifika huko na kushuhudia mambo makuu yasiyoelezeka.
Baada ya kifo na kufufuka kwa Yesu, watu waliomwamini Yesu wanapokufa huenda paradiso ya juu mbinguni wakisubiri ufufuo wa kwanza utakaotokea wakati wa unyakuo (1 Wakorintho 15:52).
Waovu wa nyakati zote tangu Agano la kale na wengine wote wanaokufa pasipo kumkubali Yesu wanabaki kuzimu wakisubiri ufufuo wa mwisho utaoambatana na hukumu ya mwisho ya kwenda jehanum ya milele (Ufunuo 20:11-15).
8 | F a h a m u K u h u s u K U R U D I K W A Y E S U
Comments
Post a Comment