KUYASHINDA MAWAZO!

1610538,DirectLink_1,22607892,https://www.profitablegatecpm.com/cmsm44evgd?key=14968b76cc3b7bd087c4ee0b9793b1a0

KUYASHINDA MAWAZO!

Sehemu ya kwanza (1)

   MAWAZO ni hali/nguvu ya ushindani kifikra inayompata Mtu/Mwanadamu katika kuchanganua hali/vipindi tofauti vya maisha anayopitia pia katika kutafakari mambo ya msingi yanayomkabili katika maisha ya kilasiku;MAWAZO ni kitu chochote ambacho mwanadamu anafikiria katika kichwa chake. Hivyo basi utagundua kua ni dhahiri Mwadadamu huyu upo uwezekano wa hali ya juu/mkubwa wa kuweza kuwaza mawazo mazuri(yenye mafanikio), pia vilevile kuwaza mawazo mabaya (yenye hasara) na kimsingi mawazo haya yenye hasara ndio yanayotesa watu wengi na kwa namna nyingi tofauti katika maisha ya wanadamu wa sasa.

   Katika kuwaza kunamajawabu yakila namna, kwamaana kuwa kila linaloonekana leo liwe jema au baya uwe na uhakika lilizaliwa kwanza katika ulimwengu wa roho usioonekana (wa mawazo) ya mtu fulani na kisha kuwapo katika ulimwengu wa nyama unaoonekana na kila mmoja kuanza kuona pia hata kutumika kwa matumizi rasmi/yasio rasmi.

   Mh! lakini kunamambo mengi watu hawajui katika siri nzito ambapo hawaelewi uhalisia wa mawazo mengi walionayo wanadamu sasaivi kua yanatoka kwa baba wa uongo ibilisi shetani, ni ukweli usio pingika kua ipo nguvu kubwa ya ushawishi katika mawazo ya wanadamu na asilimia 95% ya binadamu tunadhani yote ni mawazo/fikra zetu wenyewe, LA! hasha fikra na mawazo hayo ya ushawishi hupandikizwa na nguvu za giza na hatimaye hufanikiwa kuwateka wanadamu wengi na kuwaweka katika mikono ya ibilisi bila wao hao binadamu kutambua kua wamefungwa tayari  na hayo mawazo ya nguvu za giza na hata ukimueleza kwa haliyakawaida hawezi kuelewa (mwanadamu huyu aliekamatwa tayari) kwakudhani yuko sahihi kwa mawazoyake hayo yaliyopandikizwa katika fahamu zake.

VISHAWISHI VYA MAWAZO

Vishawishi vya mawazo ndio njia na mbinu pekee ambayo shetani hutumia kuwateka wanadamu.Hapa nitazungumzia vishawishi vya mawazo ambavyo shetani hutumia kukwamisha/kuwaangusha wakristo waliookoka. Kimsingi nguvu za giza hutumia sana mawazo kumwingizia mtu mapepo na roho chafu katika akiliyake/mawazo ya mwanadamu. kwanjia nyingine hii ni njia ya kupenyeza mawazo fulani  kwenye kichwa cha mtu au watu, ili baada ya muda fulani yaweze kuzaa matendo halisi. KWAMFANO; kuawakati mtu unaweza kujikuta unaimba wimbo flani katika mawazo na ghafla/mara unasikia mtu wa pembeniyako nae kwawakati huohuo anaimba wimbo huohuo unaouwaza wewe katika akili/ufahamu... wako.Huu ni mfano mzuri wa mvutano wa mawazo. Na nidhahirikua mawazo yanaweza kuhamishwa kutuka mtu mmoja hadi mwingine bila kuonekana kimwili. Na ni uhalisia kua mawazo yanaweza kuhamishwa kutoka mtu mmoja hadi sehemu alipo mwingine wala haitegemei umbali katika ulimwengu wa roho
 Hivyo mawazo ya mtu aliyeko TANZANIA yanaweza pokelewa na mtu alieko UGANDA,AMERIKA,ULAYA na sehemu nyingne popote alipo mlengwa wa kufikiwa na mawazo hayo; Nidhahiri kabisa ibilisi anatambua na kuelewe namna hii ya utendajikazi kimawazo hivyo basi uwe na uhakika hata nguvu za giza huweza kutumia ujuzi huo kumletea mtufulani mawazo mabaya/machafu. Yaani kwa rugha nyepesi na rahisi kueleweka ni kwamba mapepo yanao uwezo mkubwa wa kumchezea mtu kupitia mawazoyake, na kumfanya mtu huyo afike kwenye eneo la hatari ambapo mtu hujikuta ghafla ametekwa na hali ya dhambi na dhahiri kuonyesha mawazoyake katika matendo kama tu hauna nguvu na uweza wa BWANA YESU KRISTO ndani yako.
   NJIA RAHISI NA YAPEKEE YA MTU KUSHINDA MAWAZO YA USHAWISHI ni kuyaelekeza mawazo ya moyo wako katika mambo ya YESU KRISTO PEKEYAKE. Ukae ukiwa unafahamu hili dhahiri maana ni uhalisia katika ulimwengu wa roho, kwamba katika vita vyetu dhidi ya wakuu wa giza kuna roho mbaya na chafu hutumwa kutoka kwa wakuu wa mapepo na nawakalawake kwenda moja kwa moja kwa wakristo wanaoishi katika Dunia hii.                            {Kuna kitabu kimoja kinaitwa MKUU WA WACHAWI SASA AMPOKEA KRISTO mwandishi IYEKE NATHAN UZORMA sehemu ya kwanza. nna nukuu uk.124juu ameandika "Katika vita vyetu juu ya wakuu wa giza, kunaroho chafu nyingi ambazo hutumwa kutoka kwa Elam,pepo mkuu anaeishi katika njia ya Retz uliopo katika sayari ya Venus, kwenda kwa wakristo wanaoishi katika dunia. Hii hufanyika kila jumapili saa sita usiku. Roho hizo hutumwa kwa mawakala wa kibinadamu ambao huzitumia kuwashawishi na kuwakwaza waumini kwa njia mbalimbali. mwisho wa kunukuu}
      Kwa namna moja au nyingine mkristo ulie okoka usilegeze kamba kaza zaidi maana vita ni kali na shetani amejipanga haswa kuyachezea mawazo na fikra za watumishi wa mungu
kisawasawa hivyo hatuna muda wa kukaa kizembe tunatakiwa kupambana sana katika ulimwengu wa roho iko vita isiyonyamaza kabisa. Na tuzidi sana kuyaombea mawazo yetu kamwe yasiweze kupandikizwa mawazo machafu ndaniyetu kwamaana shetani anaujuzi na utaalamu wa hali ya juu kwa wale wasio na siraha za kiroho kwao na wanajiita wakristo wako hatrini maana kumkataashetani bila kuvaa silaha za MUNGU katika BWANA WETU YESU KRISTO ni sawa na kujitosa katika bahali hali huwezi/hujui ujuzi wowote kwa habari ya maji hayo uliojitosa kwayo. 


<script async src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-5030735873453842"
     crossorigin="anonymous"></script>




christianmyeya

Comments

Popular posts from this blog

UCHAWI KIUHALISIA

NDOTO NA MAANA ZAKE

UHALISIA ROHONI