ULIMWENGU WA MAPEPO

src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-5030735873453842"
     crossorigin="anonymous"></script>

UONGO UNAO ENEZWA NA MAPEPO


Na hapo ndipo nilipo pandishwa cheo, katika ulimwengu wa mapepo naam katika ngazi ya tatu ambayo hujulikana kwa jina la "Shira 999", hali ni mnamo mwaka 1979 na ndipo nlipo pewa idadi ya juu tena ya watumishi wa kunitumikia na kua na idadi wa watumishi wa kimapepo walioko chini yangu elfu sitini (60,000) na nikiamini mimi ndio top wa mapepo yote wakati huo sikua nnatambua kama ningepanda cheo tena kwasababu mambo ya shetani mpaka uyafikie ndipo unaujua ukweli pasipo kuyafikia huwez tambua uhalisia huo hivyo mwanzoni kabla sijatunukiwa ngazi ya Shira nilikua nnafahamu hakuna ngazi nyingine juuyangu. {haya ni maneno yaliyo nenwa na mtumishi wa mungu IYEKE NATHAN UZORMA ambae alikua mmoja wa miungu ya shetani na sasa amekombolewa KWA DAMU YA YESU na hayuko kifungoni tena).

Inaendelea......
 Wakati huo nikiwa katika mkutano huo wa kimapepo, Katika hotubayake "Elam (pepo kiongozi mkuu katika ngazi ya shira)" alituambia kua jina la siri la Yesu lilikua ni Yesu Ajonichim, na akanukuu katika biblia maneno yaliyo andikwa "Nae anajina lililo andikwa asilolijua mtu ila yeye mwenyewe"(Ufunuo 19:12) Alidai kuwa Ajonichim ni jina la siri la nafsi ya pili ya Yesu, alilopewa wakati akitunukiwa ngazi ya pili ya kipepo inayojulikana kwa jina la Kal 666 na kwamba kiongozi wake wa kiroho alikua Zadok.
Elam alitujulisha kua hadi leo YESU anaendelea kuteseka huko Kosa (kosa ni gereza la kipepo ambalo lipo huko Retz) alisema amkosa hayo ni adhabu ya yeye kufanya makosa alipokua duniani kama binadamu. Elam alitoa mfano kua, Yesu alikua amefikia ngazi ya pili ya vyeo vya nguvu za giza, lakini alivunja viapo kwa kufanya kinyume na maagizo ya kiongozi wake Zadok, na akaanza kufanya miujiza mbalimbali huko duniani bila ruhusa ya viongozi wa nguvu za giza. Elam akaendelea kusema kutokana na makosa hayo makubwa na mengine mengi madogomadogo, Zadok akawa na uwezo wa kumuondolea Yesu uwezo wa kufanya miujiza, kiasi kwamba wakati wa kufakwake msalabani akalia akisema  "Mungu wangu wa Zadok na roho zote za Herosi mbona umeniacha?"
Elam alidaikuwa hayo ndio yalikua maneno halisi ya Yesu pale msalabani, akatuambia kua biblia haikutoa tafsiri iliyo halisi iliposema kwamba "MUNGU WANGU, MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA?(Mathayo 27:16). Elam akaendelea kusema Yesu ataenelea kua kifungoni kwa miaka 300ijayo,Elam alaendelea kusema kua Yesu alihukumiwa katika ufalme wa anga na kutupwa jela huko kosa mwaka wa 72 baada ya kristo, na baada ya hapo alituonya vikali kua yeyote adhabu kama ya Yesu itampata endapo tu atavunja siri na viapo alivyovifanya. Mafundisho hayo na mengine mengi sana yanayoambatana na hayo yanaonyesha kufuru kubwa sana dhidi ya mkombozi na BWANA WETU YESU KRISTO, kwamaana Imeandikwa katika Ufunuo 13:5-6 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya kukufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arubaini na miwili. 6Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
Elam akaendelea kusema  huku akisisitiza vikali kua Wafuasi wote wa Yesu kristo ni waalifu ambao wanatafutwa vikali ili kuahdibiwa na Mungu, kwa mujibu wa Elamu anasema wakristo hao wanajaribu kutumia maombi usiku na mchana ili kutaka kumtoa yesu kifungoni. Elam alisisitiza na kusema kua nijukumu letu sote wenye nguvu za juu, kufanya kazi kama police wa juu kuwakamata Wakristo hao na kuwaleta mbele ya Mungu Naga, ambate ndiye Mungu wa kifo na adhabu kwa wanadamu
Elam akaendelea kusema hiyo adhabu dhidi ya wakristo isingeendelea kuwepo endapo tu wangekubali na kuacha kuomba pia kuamini kwamba Yesu atatolewa pale tu atakapo maliza kutumikia adhabuyake .Akasisitiza tena akasema na wakristo kuamini kua YESU alikufa kwaajili ya dhambi za wanadamu nikosa lingine  kubwa sana, kwasababu YESU hakufa kwaajili ya dhambi ya mtu yeyote ispokua dhambizake mwenyewe.
Pia katika mkutano huo pia Elam alituambia ninini sala za waumini wa KRISTO YESU kutoa moshi katika ulimwengu wa roho, alisema kua moshi ulitokana na ukweli wa sala kama hizo hazikuweza kutimiza malengoyake ya kumfungua Yesu kutoka kifungoni, hivyo zilibadilika na kua moshi na kuharibu kazi zingine za nguvu za giza katika ulimwengu wa roho. MTUMISHI WA MUNGU(kwasasa ambaye amemkataa shetani na kazi zake zote) IYEKE NATHAN UZORMA anasema "ukweli ni kua hotuba ya Elam ilinifanya niamini (kwasababu imani huja kwa kusikia) na kuanza kupambana kwa kasi na ari mpya dhidi ya wakristo kwakudhani kua kwawakatiule nilikua nnafanya kazi nzuri ya kumpendeza mungu na mtu. IMEANDIKWA katika Yohana 16:2-3  2Watawatenga na masinagogi; naam, saa inakuja kila mtu awauaye atakapodhania ya kuwa anamfanyia Mungu ibada. 3 Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.
 Baada ya hapo Elam alitueleza habari za kiumbe anaeitwa Jehova, Alituambia kua kulikua na kundi la Roho za giza zilizojulikana kwa jina la Sheres, ambazo zilikua na nguvu sana katika ulimwengu wa roho. Kundi hilo baadae wakamriwa na mfalme wa anga kuwa waende duniani kuendeleza jamii ya binadamu. Roho hao baadae wakatokea duniani na kuishi kwa mimilioni ya miaka kabla ya Adam na Eva, Elam akasema wakati wakiwa duniani hao Shares waliapa kutotumia nguvu zao za juu hivyo wakarudisha nguvu zao za juu kwa mkuu wa anga na kutengeneza kitu kama umbo la mwanaume mwenye nguvu ili kuwalinda wangali hapa duniani. Hao shares hatimae wakaondoka na kwenda kuishi huko Lumani kwenye kanda ya ufalme wa majini. Tena Elam akaendelea kwakusema kua, wakati wa Adam hao Shares walikua kule majini walizaliwa duniani kama uzao wa Waebrania. Wakati huo ile alama ya "mwanaume" kule angani ilikua inaabudiwa kama mungu mdogo na hilo umbo baadae likajifunua kwa Musa kama Yehova wa zamani. Na kutoka wakati ule, Yehova (yaani lile umbo) akawa Mungu wa waebrania.        MWISHOWE Elamu akatuambia wote twende kule aliko Yehova na Yesu Ajichonim, ili kujionea yote aliokua anatuambia...... ( ni sehemu ya nukuu ya kitabu cha  MKUU WA WACHAWI SASA AMPOKEA KRISTO by IYEKE NATHAN UZORMA  


Ni ukweli usiopingika kabisa Shetani Ibilisi ambae ni baba wa uongo yuko kazini vikali kupigana katika ulimwengu wa Roho edha uwe unajua au hujui au unapigana katika ulimwengu wa roho au umebweteka ukweli ni huu kwamba vita ya Shetani juu ya WAKRISTO TULIOOKOKA ni kali sana katika ulimwengu wa Roho na SIO kuokoka tu ukisha jitangaza wewe ni MKRISTO shetani anapambana vikali na wewe tena kwa njaa yakukuua kabisa hivyo sio muda wakuupoteza hali haupo katika maombi na kuzivaa kikamilifu zile silaa za imani hii ya BWANA NA MWOKOZI WETU YESUKRISTO.
<script async src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-5030735873453842"
     crossorigin="anonymous"></script>
<script async

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

UCHAWI KIUHALISIA

NDOTO NA MAANA ZAKE

UHALISIA ROHONI