NAMNA YA FANYA MAAMUZI YA HEKIMA HASA UKIWA KIJANA.

 NAMNA YA FANYA MAAMUZI YA HEKIMA HASA UKIWA KIJANA (somo na Mwl.Christian Myeya)

Joshua 24:15.
15. And if it seem evil unto you to serve the LORD, choose you this day whom ye will serve; whether the gods which your fathers served that were on the other side of the flood, or the gods of the Amorites, in whose land ye dwell: but as for me and my house, we will serve the LORD.
Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.

      NINA KUOMBEA KWA MUNGU BABA KUPITIA BWANA NA MWOKOZI WETU YESU KRISTO ALIYE HAI UWEZE KUYAELEWA YOTE KWA MAPANA MAKUBWA YA ROHO MTAKATIFU USOMAPO SOMA HILI AMINA. Basi atika  somo letu hili ili kuweza kueleweka kirahisi zaidi nianze na kutoa maana za maneno yaliyoko katika kichwa cha somo hili:-

MANENO HAYO YALIYO UNDA SOMO NI,

1.Maamuzi

2.Hekima

3.Kijana

MAAMUZI NI NINI?

   Maamuzi ni hatma/wazo la mwisho kabla ya kuingia katika hatua ya utekelezaji. (hili ni jambo nyeti sana kwamaana Maamuzi kwa wasio na misimamo huwa yanatabia ya kuyumbishwa na kubadirika-badirika, yaani kutokua na msimamo wa ki-mawazo kabla ya kufanya jambo kusudiwa) 
         :-Ni picha ya mwisho wa jambo lililopo akilini/kwenye fikra kabla halijaanza kufanyiwa kazi. (maranyingne picha hii haionekani vizuri/hutatanisha)
 Wako baadhi ya watu husema HUYU ANA-MAAMUZI MEPESI-MEPESI SANA, MWINGINE ANA-MAAMUZI MAGUMU SANA, wengine husema ANA-MAAMUZI YA HARAKA SANA, labda tena HANA-MAAMUZI MAZURI KABISA, HAWEZI KUAMUA MAMBO, tena ANA-MAAMUZI YA KITOTO, MAAMUZI YA KIKE/KIUME. nk......(haya yoooote hutokana na picha aliyoibeba mwenye Maamuzi humpelekea kupewa jina moja wapo kati ya hayo ama zaidi ya hayo niliyo yaandika maana ni mengi majina ya wenye Maamuzi)
 Ni Nini basi hupelekea wewe kama mwanadamu kuambiwa au kuwekwa kwenye kundi mojawapo la wana maamuzi hawa!? NI NAMNA YA WEWE UNAVYO WEZA KUAMUA MAMBO KI-BINAFSI au KWAAJILI YA KUNDI/WENGINE.

 MAAMUZI BORA,MEMA/MAZURI

Maamuzi haya ni yale yanayobeba hatma(hitimisho) zuri lililo na faida pia lakufurahiwa kwa binafsi hata wengine wengi kufurahia kikamilifu.
Rejea Biblia Takatifu;- kumbukumbu la torati 16:19.

Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki.

kumbukumbu la torati 25:1.

pakiwa na mashindano kati ya watu, wakaenda maamuzini, na hao waamuzi wakawaamua; na wampe haki mwenye haki, na wamhukumie makosa yule mwovu; (kumbuka huangalia hatma, katika mstari huu mwishoni Kuna hukumu)

kumbukumbu la torati 16:18.
Weka waamuzi na maakida katika malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako; nao wawaamue watu kwa maamuzi ya haki. (Katika kila jambo ufanyalo amua jambo kwaajili ya Bwana na watu woote wanao kuzunguka hakika waseme/waamue mioyoni yakwamba ni haki kwaajili ya Bwana.)

Description

In psychology, decision-making is regarded as the cognitive process resulting in the selection of a belief or a course of action among several possible alternative options, it could be either rational or irrational.

  HEKIMA
  Hekima ni Uwezo wa kufikiri kwakina na kutenda ubusara/umakini huku kitumia ujuzi,uzoefu,mawazo pevu pia hali kubwa ya uelewa.
  HEKIMAni hali bora ya mtu katika kutambua ukweli wa binadamuvitumatukio na mazingira mbalimbali hata kuchagua vizuri la kufanya.

 HEKIMA ni uwezo wa ndani (wa kufikiri na kutenda kwa kutumia ufahamu, uzoefu na maarifa) unaoambatana na roho (chanzo kisichoonekana) nyuma yake uletao matokeo yanayohitajika au yaliyokusudiwa.

Roho hiyo inaweza kuwa ni Roho wa Mungu au ni roho ya shetani.

Ujuzi huu ni uwezo wa kutumia maarifa na ufahamu alionao mtu ili kuleta matokeo hitajika yaliyokusudiwa.

Kumbe kwa maana hii tunaona sasa; kuna aina mbili za HEKIMA.

1~ Hekima ya Mungu
2~ Hekima ya dunia

Hivyo basi turudi kwenye somo husika tulilonalo hii leo (NAMNA YA KUFANYA MAAMUZI YA HEKIMA UKIWA KIJANA) hapo nilitaka tupate maana ya neno hekima na kisha kuendelea.....

KIJANA

   kijana ni mtu yoyote wa kike au wa kiume mwenye umri kuanzia miaka 18-35[45], ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni ,kisiasa na kisheria ana uwezo wa kujitegemea na kujiamulia kufanya maamuzi yake binafsi.

MAMBO MUHIMU YANAYO MUELEZEA KIJANA.

UTAMBUZI.
Kijana ni lazima awe na utambuzi binafsi {personal recognition}, utambuzi wa jamii yake na mazingira yanayomzunguka. Kujitambua kunamfanya kijana kufanya mambo sahihi na kuenenda sawa na maadili ya jamii na taifa kwa ujumla. Hivyo basi kijana sio idadi ya namba tu bali kijana ni Zaidi ya namba za umri ulizonazo kwa kujitambua wewe mwenyewe kwanza na kutambua mazingira yanayokuzunguka. Hivyo basi kijana yoyote wakitanzania anapaswa kujitambua hii ni silaa kubwa sana katika maisha ya ujana.

MAAMUZI.
Maamuzi ni chaguo analofanya mtu, chaguo hili linaweza kuwa sahihi au lisiwe sahihi. Lakini maamuzi ni matokeo ya mawazo ya kitu Fulani.

Hivyo basi hatua yoyote ya maamuzi kwa kijana kwenye maisha yake, huweza kuleta matokeo sahihi au yasiyo sahihi. Kijana ni muhimu kuwa mtu wa tofauti na kufanya maamuzi sahihi kwani maamuzi unayoweza kufanya leo yanaweza kukusaidia na kufanya maisha yako kuwa mazuri au kuharibu ujana wako na maisha yako kwa ujumla. Maamuzi ni sumaku inayovuta kutenda mabaya au mazuri, kama kijana chagua kutenda mema kwani kesho yako huwa halisi unapofanya maamuzi sahihi leo.
UWELEWA WA CHANGAMOTO
Ni lazima kijana aelewe changamoto mbalimbali na kujua jinsi ya kukabiliana nazo, kwani changamoto huwa hazikimbiwi ila tuna zitatua au kuzipunguza kwa namna salama. Kumekuwa na vijana ambao huchukulia ugumu wa changamoto hizi kutenda mambo mabaya kama kujiingiza katika vikundi vya kigaidi, uvutaji bangi na madawa ya kulevya kwa ujumla. Kama kijana halisi na anayejitambua atachagua njia salama za kutatua na kukabilana na changamoto. Matatizo haya au changamoto ni kama ukosefu wa ajira kwa vijana wengi hasa pale wanapomaliza elimu zao, kukosa elimu ya stadi za maisha, elimu ya afya nk.

KUJENGA HOJA.
Umri mzuri wa kuwa na hoja na zenye nguvu katika masuala mbalimbali ni kijana. Ni lazima uwe mwepesi kushiriki masuala mbalimbali ya kujenga hoja hasa zenye maslahi mapana kwa jamii inayokuzunguka au taifa kwa ujumla. Kujenga hoja, kutetea na kupinga hoja zisizo na mashiko kwa vijana wa kitanzania kwa kufanya hivi kijana anajenga nafasi nzuri ya kusikilizwa na jamii lakini pia kuaminiwa kwa ushawishi wa hoja katika umri wako wa ujana.

USHAWISHI.
Kijana ni lazima awe na ushawishi katika masuala muhimu na kwa manufaa ya jamii kwa ujumla hasa kwa vijana wenzake, katika kushawishi ndio tunaona nguvu ya kijana na kuanza kutengeneza taifa imara. Vijana wengi kwa sasa tunajitahidi sana kuwa na nguvu ya ushawishi, pia tunaona asasi nyingi zikiongozwa na vijana wenyewe ili kuweza kushawishi mambo yenye tija kwa maisha ya vijana. Lakini pia hata serikalini vijana wengi wameaminiwa na kuoesha ushawishi mkubwa sana kuwa wana uwezo wa kufanya kazi na hivyo kuaminiwa na serikali.

UKOMAVU WA AKILI.
Kuwa na akili ya kufanya mambo yanayoendana na umri wako. Vijana wa kitanzania ni lazima waendane sawa na umri wao hii itasababisha hata kufanya mambo makubwa Zaidi katika jamii na yenye matokeo chanya, wawe na uwezo wa kumshauri kijana au vijana wenzao, familia au jamii husika kwa kutoa dira kwa vijana wenzao, hii itaambatana na kupanga mipango na kuanza ufuatiliaji ili mipango itimie kama vile kubuni wazo Fulani lenye lengo/manufaa kwa kijana au kwa jamii, biashara au kufikiria kazi nzuri anayoweza kufanya. Lakini kufanikisha hayo kijana ni lazima;-

KIJANA LAZIMA ATAMBUE MAMBO HAYA;

AJITAMBUE.
Kijana lazima ajitambue na kutambua fursa mbalimbali zinazomuhusu,
Unapojitambua ni lazima ujue thamani yako na kusudi la uwepo wako, kwa kujitambua unaweza kufanya mambo mazuri sana kwa jamii na taifa kwa ujumla.
AJIKUBALI
Kujikubali ni hali ya kupokea mambo yote yanayokuhusu, kijana anapaswa kujikubali jinsi alivyo hii itamsaidia kusonga mbele Zaidi. Mfano mtu una tatizo Fulani na ambalo linakufanya tofauti na wengine unapaswa kujikubali, ili ujione kuwa ni wa thamani kama wengine walivyo.Kwani unapojikubali unaweza kujiona wa kawaida na kufanya mambo makubwa kwa familia,jamii na taifa kwa ujumla, na kufanya utambulike na unaweza kuwa mfano wa kuigwa.
AWE NA SHAUKU,NIA NA KIU.
Kijana ni lazima awe na awe na shauku nia na kiu ya kufanya vitu tofauti tofauti venye lengo la kuelimisha au kutimiza kusudi, maono au matarajio yao.
AWE MZALENDO.
Kijana anapaswa kuwa mzalendo sana, hapa kama kijana inabidi ujiulize na kujua kusudi la kuwepo Tanzania. Ni lazima ujue unapaswa kuwa mzalendo kwa nchi yako. Ufanye yaliyo mazuri kwa nchi yako, ufanye yaliyo mazuri kwa jamii yako ya kitanzania.
MAMBO YANAYOMBEBA KIJANA

NIDHAMU.
Nidhamu ni uwezo wa kufanya mambo/vitu Fulani pasipo kufuata hisia[ kinyume na ulivyozoea]. Kijana/ujana ni lazima uambatane na nidhamu ya hali ya juu ili aweze kuvuka vikwazo mbalimbali.
HESHIMA.
Ni hali ya ndani ya uthamani anaokuwa nao mtu kwake na mwingine au ujali wa kuangalia rika kujenga uthamani na hii tunaweza kusema ni asili ila jamii wanaijenga au wazazi wanaijenga ili ushirikiano uwepo. Hivyo basi heshima utakayoionesha wakati wa ujana wako ndio itakayokusaidia/kukubeba katika maisha yako ya ujana mpaka uzeeni.
UWAJIBIKAJI.
Ni hali ya kiongozi na mtendaji kuwa tayari kubeba dhamana na kutoa maelezo kwa wananchi juu ya maamuzi au matendo aliyoyafanya katika kutekeleza dhamana aliyopewa. Hivyo basi jifunze kuwajibika katika majukumu mbalimbali ili ufanikiwe, msingi wa maisha yako ni lazima kufahamu namna ya kujiandaa na maisha yako ya baadaye. Uwajibikaji katika uongozi hadi maisha ni moja ya misingi na nguzo mama inayotubeba kama kijana, kwani uwajibikaji bora huleta matokeo chanya kwenye kila wazo,mpango au maono Fulani.
UADILIFU.
Ni hali ya kuwa mwaminifu na kuwa na mwenendo mzuri katika utendaji kazi au kitu chochote kile. Uadilifu unahusisha kujali watu, kujali muda, kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na kuwa mkweli. (tusizidi sana mbele twende katika kiini cha somo letu 

(NAMNA YA KUFANYA MAAMUZI YA HEKIMA HASA UKIWA KIJANA)

Sasa nadhani kwaupana mkubwa wa neno moja baada ya lingine katika somo hili tayari umepata nitazungumza machache yakukufanya kuelewa kwa undani zaidi na kukusaidia kufanya maamuzi yenye hekima ya ki-MUNGU kila wakati kila saa, Karibusanatuendelee...

Comments

Popular posts from this blog

UCHAWI KIUHALISIA

NDOTO NA MAANA ZAKE

UHALISIA ROHONI