NAMNA YA KUFANIKIWA HARAKA.

    <script async src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-5030735873453842"

     crossorigin="anonymous"></script>

 SHINDA TABIA HIZI ILI UMUONE MUNGU


 (a)TABIA YA KUJIHURUMIA HURUMIA


Kamwe Hakuna Mafanikio Kwa Watu wanaojihurumia kwenye kufanya mambo,Watu wanaojihurumia hurumia kwenye kumtolea Mungu Kwamba nikitoa Hii Sasa nitaishije,Sasa Nitakula Nini ,Watu wanaojihurumia kwenye Kuwa na Maisha ya Mifungo ,eti nikifunga Sana Si nitakonda , nikifunga mara Kwa mara eti nauchosha Mwili Wangu , Watu wanaojihurumia hurumia kwenye Kuomba Wanaomba kistaha staha   KAMA UNATAKA KUUONA MKONO WA MUNGU KAMWE EPUKA KUWA MTU WA KUJIHURUMIA HURUMIA FANYA MAMBO KWA KUJITOA ,FANYA MAMBO KWA KUJIDHABIHU


 (b) TABIA YA KUPENDA USINGIZI


Hata Maandiko Yanasema apendaye Usingizi huelekea Umaskini, Usingizi ni adui anayewachelewesha wengi kufikia Hatma zao, eti Wapo Watu wanafuata Ushauri Wa kidaktari Kuwa Mtu ANAPASWA kulala masaa8 Kwa Siku ,Ndugu Yangu ukipenda Usingizi hakuna Mahali ambapo utafika Bali Mtu Wa kushangilia wenzako tu Achana na mambo ya kulala lala HOVYO,Huo Muda UnaolalaTumia Muda Wako Kukaa na Mungu Kupitia Maombi, Kusoma Neno,Kusoma Vitabu,Kupanga mambo Yako Utakuwa unafanya kitu Cha Maana Sana

Nitafutie Mtu aliyefanikiwa Kiuchumi, kihuduma anayependa kulala lala ,utagundua Kila aliyefanikiwa kwenye Eneo Lolote basi ameushinda USINGIZI

MITHALI 20:13


 (c)TABIA YA UVIVU NA ULEGEVU LEGEVU


Wengine kinachowachelewesha kufikia Hatma zao Siyo Shetani Bali ni Hii tabia ya UVIVU UVIVU TU NA ULEGEVU LEGEVU , Watu wanafanya mambo kivivu vivu, Kilegevu legevu, wanaomba kivivu vivu kama vile kalazimishwa , wanafunga kivivu vivu mpka asikie TANGAZO la Mfungo Kanisani,anamtumikia Mungu kivivu na Kilegevu anatumika Bora liende tu , Kwenye Kutoa napo ni Kivivu Vivu MAISHA YANATAKA WATU WANAOFANYA MAMBO KWA BIDII NA JUHUDI KUBWA SANA ,SIYO WATU SMART SMART 


(4)TABIA YA KULA KULA


Kilichowaangusha Adamu na Eva pale bustanini ya Edeni ni Chakula,Kilichomponza Essau ni Chakula ,Hata Yesu Jaribu la kwanza lilikuwa ni Chakula aliambiwa ageuze mawe Yawe makate

Kinachowaponza Watu Wengi Sana ni Kupenda Kula Kula Badala Ya Kufunga ,Kuna Watu Hawana Nidhamu Kabisa Ya  Kufunga Hata wakifunga Wanafunga ili mradi , Wakifunga Leo Inaweza ikapita Miezi kadhaa Bila Kufunga, wengine Kufunga kwao Mpka watangaziwe na Kanisa 

SHINDA TABIA YA KULA KULA NA UWE MTU WA KUFUNGA MARA KWA MARA 

MWANZO 3:....... LUKA 4:1-8


(5)TABIA YA KUTOFANYA VITU KWA MWENDELEZO


Moja Kati Ya Kinachowakwamisha Watu Wengi Sana ni Kutofanya Vitu Vingi Bila Mwendelezo , Wengi Sana wanafanya vitu Kwa Kukatisha katisha, wanafanya vitu Kwa Kuacha acha, Leo wameomba kesho hawaombi, Leo kasoma Biblia Kesho hasomi,Wiki hii kafunga inapita miezi ndiyo anafunga ,anatoa Wiki Hii Wakati Mwingine hatoi KAMA UNATAKA KUUONA MKONO WA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO BASI JIFUNZE KUFANYA VITU KWA MWENDELEZO HATA KAMA HAUONI MATOKEO WAKATI HUO UNAOFANYA LAKINI USIACHE KUFANYA


(6)TABIA YA KURIDHIKA


Tabia nyingine ambayo ni Kizuizi Cha Watu Wengi Kutumuona Mungu Kwenye Maisha Yao ni KURIDHIKA  


Wengi Sana Wameridhika na Maisha Waliyonayo , Wengi Sana Wameridhika na Viwango Vya Kiroho walivyonavyo ,wengi sana Wameridhika na aina Ya Maisha Wanayoishi Ndiyo Maana hawatafuti Kutaka Kwenda Viwango Vingine, Ndiyo Maana hawafanyi Bidii Kubwa Ya Kutaka Kupiga hatua Zaidi ,


KAMWE KATAA KURIDHIKA NA AINA YA MAISHA ULIYONAYO,KATAA KURIDHIKA NA KIWANGO CHA KIROHO ULICHONACHO,KATAA KURIDHIKA NA AINA YA MAFANIKIO ULIYONAYO NA TAFUTA KUFANIKIWA ZAIDI, TAFUTA KUPIGA HATUA ZAIDI, TAFUTA KUSONGA MBELE ZAIDI, TAFUTA KUMJUA MUNGU ZAIDII

WAFILIPI 3:12-14

Comments

Popular posts from this blog

UCHAWI KIUHALISIA

NDOTO NA MAANA ZAKE

UHALISIA ROHONI