KURUDI KWA YESU MARA YA PILI SEHEMU YA KWANZA
KURUDI KWA YESU MARA YA PILI SEHEMU YA KWANZA Ujio wa Yesu kwa mara ya kwanza kama kulivyotabiriwa kulikamilika kwa kupitia kuzaliwa na bikira Mariamu. Aliishi kwa makusudi maalumu ya kuleta ukombozi kwa njia ya kifo pale msalabani (Marko 10:45). Wakati maisha na huduma yake hasa wiki ya mwisho aliongea habari za kuondoka lakini kwamba angerudi tena (Yohana 14:1-4; Mathayo 24:4-31). Baada ya kumaliza kazi hiyo msalabani alipaa na kwenda kwa Mungu Baba na malaika waliwakumbusha wanafunzi wake kwamba huyo Yesu waliyemwona anapaa atarudi tena (Matendo 1:11). Kurudi kwa Yesu ni fundisho la msingi la imani ya kikristo ambalo ni tumaini lenye baraka. Fundisho hili huleta hamasa na shauku ya kumngoja Yesu kwa hofu na utakatifu hali tukimtumikia Mungu kwa juhudi kwa sababu ushirika wa sasa na Kristo una uhusiano na matokeo makubwa sana katika maisha yajayo ya milele. Kuja kwa Yesu mara ya pili vi | F a h a m u K u h u s u K U R U D I K W A Y E S U ...